Breaking News

RC Makonda kasitisha bomoabomoa ya zaidi ya nyumba 17,000

on

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda leo August 30, 2017 ametembelea Bonde la Mto Msimbazi lililopo katika Wilaya ya Kinondoni ambako wananchi walitangaziwa kuwa nyumba zao zaidi ya 17,000 zitabomolewa.

RC Makonda amewaondoa hofu wananchi ambao walikuwa na hofu ya kubomolewa akisema kuwa hakuna atakayefanya hivyo kwa kuwa hawakufuata utaratibu na kuagiza kuwa atakayethubutu kufanya hivyo atachukuliwa hatua za kisheria.

>>>”Kwa sababu hawajafuata utaratibu, nasitisha ubomoaji wa nyumba DSM kuanzia sasa, Tanroad na watu wa reli wao walitoa taarifa. Yeyote ambaye ataanza kubomoa bila kutoa taarifa naomba Kamanda Mambosasa huyo mtu nimkute kituo cha Polisi.” – Paul Makonda.

“Hakuna atakayewabomolea nyumba zenu” – RC Makonda

Tupia Comments