Premier Bet
TMDA Ad

Top Stories

Hesabu za Mwinyi Zahera baada ya Congo kukalia kuti kavu AFCON 2019

on

Kocha msaidizi wa Congo DR Mwinyi Zahera baada ya timu yao ya taifa kuwa na nafasi finyu ya kusonga mbele katika michezo ya fainali ya AFCON 2019, Mwinyi Zahera ameeleza kuwa timu yake ilizidiwa na kupoteza nafasi tatu za wazi hivyo sasa mawazo yake yapo katika best Looser.

Zahera ameeleza kama Congo DR ikimfunga Zimbabwe itakuwa na point tatu na inaweza kusonga mbele kwa nafasi ya Best Looser, kwani Kundi lao A hawawezi kupata nafasi ya pili hata wakishinda mchezo wao wa mwisho dhidi ya Zimbabwe kutokana na Misri wana point 6 na Uganda wanazo 4.

Timu ya taifa ya Congo ambayo imewahi kuchukua taji la AFCON mara mbili katika historia, kwa sasa imekuwa haifanyi vizuri kwa miaka mingi na imekuwa ikisuasua toka 1974 ilivyotwaa taji hilo kwa mara ya mwisho na msimu huu inaonekana kama imemaliza hivi.

VIDEO: Inabidi Muielewe tu Taifa Stars, Msuva Kaongea Kwa Hisia

Soma na hizi

Tupia Comments