Timu ya taifa ya Tanzania kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 leo May 18 2017 katika uwanja wa Stade de Amitie Libreville Gabon waliingia uwanjani kucheza mchezo wake wa pili wa Kundi B wa michuano ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 dhidi ya timu ya taifa ya Angola.
Serengeti boys wameingia uwanjani kucheza game yao ya pili baada ya mchezo wao wa kwanza wa Kundi B kucheza dhidi ya Mali ambao ni mabingwa watetezi na kulazimishwa sare tasa 0-0, sare dhidi ya Mali iliwafanya Serengeti Boys kuingia katika mchezo dhidi ya Angola kwa nguvu zaidi ili kupata ushindi na kujiweka katika nafasi nzuri ukizingatia kabla ya michezo ya leo timu zote zilikuwa na point moja moja.
Tanzania leo wamefanikiwa kupata ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya timu ya taifa ya Angolaukiwa ni mchezo wao wa pili wa Kundi B lenye timu za Niger, Mali na Angola, magoli yaSerengeti Boys yalifungwa na Kelvin Nashoni dakika ya 5 na kipindi cha pili dakika ya 69 Abdul Hamis Seleman akaifungia goli la ushindi Tanzania baada ya Angolakusawazisha goli la kwanza dakika ya 17 kipindi cha kwanza kupitia kwa Pedro.
Ushindi huo wa Serengeti Boys umewafanya waongoze Kundi B wakati wakiwa wanasubiri matokeo ya mchezo wa Mali na Niger, Serengeti wana point nne hadi sasa na ili kufuzu hatua ya nusu fainali ya michuano hii wanahitaji sare dhidi ya Niger mchezo wa mwisho watakaocheza Port Gentil, Tanzania wakifuzu nusu fainali ya AFCONwatakuwa wameingia moja kwa moja katika fainali za Kombe la dunia zitakazochezwa India mwishoni mwa mwaka 2017.
VIDEO: Alichoamua Rais wa Simba baada ya kupokwa point 3 na TFF vs Kagera