Inaripotiwa kuwa rapper Cardi B amekana mashtaka yake yote mawili dhidi yake ni kwenye kesi ya kuwapiga na kuwafanyia fujo wasichana wawili kwenye ukumbi wa starehe ‘Angels Strip Club’ mjini New York usiku wa mwezi August 2018.
Inaelezwa kuwa Cardi B alisimama kizimbani June 24,2019 na kukana mashatka hayo kwenye Mahakama Kuu ya Queens County Criminal Court iliyopo mjini New York, Cardi B alisikika akimuambia Hakimu Joseph Zayas ”Sina hatia”.
Inadaiwa kuwa Cardi B alianzisha fujo katika ukumbi wa Angels Strip Club mwaka 2018 ambapo aliwarushia viti wasichana wawili ambao majina yao yanatajwa kuwa ni Rachel Wattley na Sarah huku akiamini kuwa Rachel aliwahi kuwa mapenzini na mume wake Offset kitu ambacho kimeelezwa kuwa sio kweli.
VIDEO: MAMBO SHWARI!! AlIYEZICHAPA NA TID KAZUNGUMZA “TULIWEKWA KATI TUKAPATANISHWA, NIWASHIKAJI”