Mwanadada Mandy ambaye ni mzazi mwenza na Davido ameweka wazi kuhusiana na ujumbe aliomtumia Female rappa Cardi B kwenye mtandao wa instagram na kumtaka siku ampe nafasi ya kumuwekea kope za bandia.
Mwanadada huyo ambaye anajishughulisha na biashara ya kuwaweka kope bandia wanadada akiwa ni mzaliwa wa Togo na Cape Verde anatamani ndoto yake itimie kwa rappa Cardi B ambapo amonekana kutokata tamaa huku akiendelea kusubiri jibu kutoka kwa rappa huyo na kuamini ndoto yake itatimia.
Kupitia instagram story Mandy ameandika ” Bado namsubiri Cardi B kunjijibu ujumbe wangu niliyomtumia ili nikamtengeneze kope zake”
Davido na Mandy waliwahi kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi miaka kadhaa iliyopita na walifanikiwa kupata mtoto mmoja wa kike.
EXCLUSIVE: “SUMU NDIO CHANZO CHA MIMI KUUMWA” – OMMY DIMPOZ