Kwa takriban siku tatu sasa, meli iliyokuwa imebeba mafuta baada ya kugongana na meli nyingine na moto mkubwa kuwaka huko Pwani ya China, moto huo bado unaendelea kuwaka huku jitihada za kuuzima zinazofanywa na vikosi vya uokoaji zikizidi kuwa ngumu.
Hii ni kutokana na hali ya hewa katika eneo hilo kuzidi kuwa mbaya kufuatia moshi mzito na mawimbi ya hadi mita 4 yaliyo katika eneo hilo huku ikielezwa kuwa meli hiyo iko hatarini kulipuka muda wowote na kuzama kabisa.
Meli hiyo ya mafuta iliyokuwa imebeba mafuta tani 136,000 ambayo inamilikiwa na watu wa Iran iligongana na meli ya watu wa China siku ya Jumamosi usiku majira ya saa mbili na kusababisha raia wa Iran 30 na Wabangladesh wawili kupotea na hadi sasa wanahofiwa kufariki, huku watu 21 waliokuwa kwenye meli ya Wachina wakifanikiwa kuokolewa.
”Nimeondoka mwenyewe, sijafuata vyeo, Nilikuwa na cheo kikubwa CHADEMA” Muslim Hassanal