Moja ya watu waliokuwa karibu na Mwanasiasa Mkongwe Mzee Kingunge Ngombale Mwiru ambaye amefariki baada ya kung’atwa na mbwa nyumbani kwake DSM ni Jaji Mkuu mstaafu Warioba baada ya kufika nyumbani kwa Mzee Kingunge aliongea na waandishi wa habari na kuelezea jinsi gani Kingunge alikuwa enzi za uhai wake.
“Ngombale ni wale Waasisi hasa wa TANU, TANU imeundwa mwaka 1954 na mwaka huo huo Ngombale akajiunga na walipelekwa na Chama kusoma nje alisoma Liberia, mtu aliyefanya itikadi ya Chama kufahamika ukiacha Mwalimu alikuwa Ngombale,”– Warioba
MAZISHI JUMATATU: BADO HAIJULIKANI NI DINI GANI ITAMZIKA MZEE KINGUNGE, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA.