Michezo

Ni Valencia na FC Barcelona fainali ya Copa Del Rey May 25

on

Barcelona ambao wamenyakua kombe la La Liga kwa msimu huu bado wana kazi ya kuwaridhisha mashabiki wao ambao bado wana majonzi ya kutolewa kwenye ligi ya mabingwa baada ya kuongoza kwa goli 3 katika mchezo wa kwanza na kuruhusu goli 4 kwenye mchezo wa marudiano dhidi ya Liverpool, game yao ya kesho ya fainali ya Copa Del Rey dhidi ya Valencia ni game muhimu kwao.

Mbali na morali kuwa chini Barcelona wana list ndefu sana ya majeruhi ambao miongoni mwao ni wachezaji wa kikosi cha kwanza, mshambuliaji Luis Suarez, golikipa Ter Stegen (maumivu ya goti), Ousmane Dembele (maumivu ya misuli ya nyuma ya goti ‘hamsring’) na kiungo wa kati Arthur (maumivu ya nyonga).

Hata hivyo Barcelona bado wana kikosi kizuri sana licha ya majeruhi walionao. Nahodha Lionel Messi amekuwa kwenye kiwango bora kabisa msimu huu baada ya kupachika mabao 36 katika ligi na kuisaidia timu yake kushinda taji hilo.

Kwa Valencia hii ni fainali yao ya 16 katika Kombe la Mfalme huku wakiwa wamefanikiwa kulichukua mara 7 na kupoteza fainali 9. Mara ya mwisho Valencia kuwafunga Barcelona katika fainali za Copa delo Rey ilikuwa mwaka 1958 ambapo walishinda 3-0, game hiyo kesho ni saa nne kamili usiku kupitia ST World Footbaall.

Mwacheni Salamba achukue viatu vya Ever Banega kwa ajili ya watoto wake

Soma na hizi

Tupia Comments