Premier Bet
TMDA Ad

Michezo

Ghana kwenye hatua nzuri michuano ya AFCON…

on

Football - 2011ACQ - Ghana v Swaziland - Accra Sports StadiumMichuano ya kombe la mataifa ya Afrika imeendelea hii leo kwa kushuhudia mchezo mmoja wa hatua ya robo fainali ukizikutanisha Ghana pamoja na Guinea.

Katika Mchezo huo Ghana walifanikiwa kufuzu hatua ya nusu fainali wakiwafunga Guinea kwa mabao matatu bila.

Ghana walianza kazi mapema wakifunga bao mapema kwenye dakika ya nne kupitia kwa winga Christian Atsu.

Black Stars walipata bao la pili kwenye kipindi cha kwanza mfungaji akiwa Kwessi Appiah bao ambalo liliua matumaini ya Guinea.

Mwanzoni mwa kipindi cha pili Ghana walifunga bao la tatu mfungaji akiwa Christian Atsu tena na kuikatia timu yake tiketi ya kufuzu hatua ya nusu fainali.

Nafasi ya mwisho kwenye hatua ya nusu fainali itafahamika saa chache zijazo wakati mchezo wa mwisho wa roo fainali utakaowakutanisha Ivory Coast na Algeria utakapopigwa.

Hadi sasa timu tatu tayari zimefuzu hatua ya nusu fainali nazo ni wenyeji Equatoarial Guinea, Ghana pamoja na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.

Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook

Tupia Comments