Kama ni mfatiliaji wa masuala ya kila kinachoendelea kwenye headlines kubwa kutoka Tanzania zilizofanikiwa kuteka zaidi siku chache zilizopita, ni ishu ya kasi ya Rais Magufuli kwenye utendaji wake huku akisisitiza kubana matumizi ya Serikali.
Kwenye kubana matumizi kwa sasa Rais Magufuli aliagiza pia kuzuia safari za viongozi nje ya nchi… Rais wa Ghana pia kaingia kwenye headlines, Rais huyo John Mahama amepiga marufuku viongozi wa nchi kusafiri nje ya nchi wakiwa wamepanda daraja la kwanza kwenye ndege (first class)… maana yake ni kwamba wakisafiri wanakuwa kama raia wa kawaida na sio VIP tena !!
Rais huyo ameagiza pia watumishi wa Serikali kutofanya safari zozote zisizo na umuhimu kama njia ya kubana matumizi… Waziri wa Fedha Ghana, Seth Terkper amesema Baraza la Mawaziri wako kwenye mjadala wa kupitisha Sheria ya udhibiti wa matumizi ya pesa, atakayekiuka kanuni za matumizi atasimamishwa kazi, kupigwa faini au kufungwa.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.