Michezo

Headlines za Jose Mourinho kurudi Real Madrid zilipomfikia Rais wa Madrid Fiorentino Perez alijibu hivi ….

on

Najua bado headlines za Jose Mourinho kuwa ataenda wapi au kuifundisha klabu gani bado zinazidi kushika kasi, je ataenda kuifundisha klabu ya Manchester United au Real Madrid kama inavyoripotiwa au klabu gani. Ukiachana na stori za kujiunga na Man United, mwezi October Rais wa zamani wa Real Madrid Ramon Calderon alimkaribisha kwa mara ya pili Mourinho kujiunga na Real Madrid na kusema bado ana nafasi ya kurejea.

December 23 stori zilizoandikwa ni kuwa Rais wa sasa wa Real Madrid Fiorentino Perez anapanga kutaka kumrudisha Jose Mourinho kuifundisha Real Marid, baada ya stori kufika kwake na majibu yake yalikuwa hivi “Tuna kocha mzuri Benitez na ndiye mtu tuliyemchagua, tunamuacha aendelee kufanya kazi kwa kushirikiana na wachezaji, nimezungumza na wachezaji na sio kweli kwamba hawataki kuendelea kufanya kazi na Benitez” >>>Perez

12E93578000005DC-3371540-image-a-4_1450856193676

Jose Mourinho ambaye amewahi kuifundisha Real Madrid kuanzia mwaka 2010 hadi 2013, alifukuzwa kazi na Chelsea wiki iliyopita na Rais wa zamani wa Real Marid Ramon Calderon aliwahi kunukuliwa kuwa Rafael Benitez alikuwa chaguo la nne baada ya Jose Mourinho, Joachim Low na Jurgen Klopp, hivyo baada ya Mourinho kufutwa kazi watu walijua anarudi Real Madrid.

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye TwitterFBInstagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.

Tupia Comments