Top Stories

Serikali ya Rais Kabila wa DRC iko hatarini kupinduliwa?

on

Leo January 19, 2018 Taarifa kutokea nchini DRC Congo jioni ya leo ni kutanda kwa hofu na wasiwasi kwa wananchi wa Mjini Kinshasa baada ya Jeshi kuizunguka Ikulu ya Rais Joseph Kabila.

Asubuhi ya leo January 19, 2018 Waandishi wa Habari nchini DRC Congo wamesema Kamanda mmoja wa cheo cha Jenerali aitwaye John Tshibangu ametangaza kuasi na kumpa Rais Kabila siku 45 awe amejiuzulu.

Kamanda huyo alitangaza hilo kupitia mkanda wa video ambao ulisambaa kupitia mitandao ya kijamii ambapo Kamanda huyo alimwambia Rais Kabila kuwa ana siri yake na hivyo ataitoa kama hataondoka madarakani.

Pia amemweleza kuwa ni lazima aombe msamaha kwa raia wa Congo kwa kosa la kushindwa kuiongoza nchi.

JPM ASITISHA USAJILI WA MELI MPYA, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUMTAZAMA

Soma na hizi

Tupia Comments