Baada ya Mamlaka kutangaza kwamba madini ya Tanzanite na Dhahabu ndio yanaongoza kwa kutoroshwa kutoka kwenye ardhi ya Tanzania, majibu yametolewa Mhandisi Baraka ambaye ni kaimu mkurugenzi wa idara ya uzalishaji na biashara ya madini kwenye migodi mikubwa ya kati na midogo.
Kwenye swali lililoulizwa kama viwanja hivyo vya Ndege kwenye migodi havitumiki kutorosha madini, Baraka amejibu >>> ‘Niwajulishe tu kwamba viwanja vya ndege vilivyopo Migodini vina majukumu tofauti kama usafiri wa Wafanyakazi sababu ratiba za migodi ni ngumu kutumia usafiri wa Public kwahiyo viwanja vingi vinatumika kwa safari zao‘
‘Viwanja hivi pia kipindi cha nyumba vilikua vinatumika kusafirishia mazao yanayotokana na migodi lakini kutokana na matatizo ya kiusalama kama mtakumbuka baada ya tukio la Geita kutaka kuvamiwa na kunyang’anywa dhahabu, siku hizi migodi yoote haisafirisha mali zao kwa Ndege, sasa hivi wanatumia Helikopta ambazo zinaingia ndani mgodini‘
‘Sisi tunajiridhisha vipi kwamba Helikopta hizo na ndege hizo haziibi mali zetu? Wakala umeweka Wakaguzi waliofundishwa na wako saa 24 kwenye migodi yote mikubwa na ya kati na wanafanya kazi siku zote 7 za wiki haijalishi sikukuu na Wakaguzi wetu hawakai nje, wanakaa kwenye vyumba maalum‘
Kufahamu zaidi unaweza kubonyeza play kwenye hii video hapa chini