Bado naendelea kukupa exclusive ya Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dr Jakaya Kikwete ambaye kwa sasa baada ya kustaafu yuko nyumbani kwake Msoga Chalinze akijishughulisha na shughuli za kilimo na kusimamia mifugo yake.
AyoTV ilimtembelea Rais mstaafu Dr Kikwete nyumbani kwake na kuzungumza nae vitu mbalimbali ikiwemo kutembelea shambani kwake, anakolima mahindi na kufuga ng’ombe, tukamuuliza akiwa amepumzika au baada ya kazi za kilimo ni nyimbo gani anapenda kuzisikiliza?
“Mimi nasikiliza vipindi vya radio tu Clouds vipindi vya radio tu nasikiliza mambo safi tu, nyimbo ninazozipenda zipo nyingi tu kwenye gari nasikiliza nyimbo za zamani tu za Nyboma sasa hizo nyinyi zitachosha tu kwanza Nyboma hamumfahamu”>>> Dr Kikwete
Kama hufahamu msanii Nyboma ambaye mstaafu Kikwete anasikiliza sana nyimbo zake ni raia wa Congo, alianza kuimba muziki wa kwaya kanisani kabla ya mwaka 1969 akiwa na umri wa miaka 18 kuanza rasmi kufanya muziki wa kidunia.
VIDEO: Penati ilizoipa Simba Ubingwa wa Ngao ya Hisani vs Yanga