Afisa mtendaji mkuu wa bodi ya Ligi Boniface Wambura leo alifanya mkutano na waandishi wa habari na kueleza maamuzi waliyofanya kutokana katika kamati ya saa 72 kutokana na matukio yaliokuwa yamejitokeza katika mchezo wa Yanga dhidi ya KMC.
Boniface Wambura mbele ya waandishi wa habari ametangaza kuwa kamati ya saa 72 ya uendeshaji wa Ligi Kuu Tanzania bara imefikia uamuzi wa kuipiga faini Yanga ya jumla ya Tsh milioni 6, hiyo inatokana na kutenda makosa mawili wakati wa mchezo dhidi ya KMC.
Kwa mujibu wa Boniface Wambura amesema Yanga imepigwa faini ya Tsh milioni 3 kila kosa katika makosa yake mawili, kosa la kwanza la kuingia uwanjani kwa kutumia mlango usiokuwa rasmi na pili la kutokuingia katika vyumba rasmi vya wachezaji hao wakati wa mapumziko.
Msimamo wa Samatta kuhusu hatma ya Kapombe katika mgao wa Taifa Stars