Habari za Mastaa

Steven Gerrard aipa bye bye timu ya taifa ya England

on

gerrad

Hadi sasa Steven Gerrard ameshinda mechi 38 kati ya 114 kwenye mechi za kimataifa katika muda wake wote akiwa mchezaji wa timu ya taifa. Lakini hivi leo Gerrard ametangaza uamuzi wake wa ku retire kucheza mechi za timu ya taifa na kuzifanya mechi za kombe la dunia kuwa ni za mwisho kwake.

Steven Gerrard amesema kwamba,”Nimefurahi sana kwenye kila dakika niliyocheza kuiwakilisha nchi yangu na hii ni siku ya masikitiko  kujua kwamba sitavaa tena jezi ya England kucheza uwanjani”.

Steven Gerrard aliongeza kwa kusema “Haya yamekuwa ni maamuzi magumu sana kwangu niliyowai kufanya kwenye maisha yangu. Tangu nirudi kutoka Brazil nimeongea na familia yangu, watu wangu wa karibu kuhusu maamuzi yangu”.

Tupia Comments