Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limesema kuwa ujio wa timu ya Sevilla kutoka nchini Hispania chini ya SportPesa Tanzania utaongeza hamasa na maendeleo ya mpira wa miguu nchini, TFF pia imewataka wachezaji wa Simba kutumia fursa ya mechi hiyo kuonyesha na vipaji vyao kutokana na kufuatiliwa kutoka sehemu mbalimbali.
Timu ya Sevilla FC inatarajiwa kuwasili Tanzania May 21 na baadaye kucheza mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya timu ya Simba May 23 kwenye uwanja wa Taifa kuanzia saa 1 usiku.
Rais wa TFF, Wallace Karia alisema kuwa Sevilla FC ni timu kubwa yenye historia kubwa katika soka duniani na hivyo ujio wao utawavutia mashabiki wa soka hata wa nchi jirani ili kuja kushuhudia wachezaji nyota wa wanaocheza bara la Ulaya.
“Walianza na ujio wa timu ya Everton ambayo ilicheza mechi kwenye uwanja wa Taifa dhidi ya timu ya Gor Mahia ya Kenya. Mastaa kama Wayne Rooney na wengine kibao walicheza kwa mara ya kwanza Tanzania na kuleta hamasa,” >>> Karia.
Sevilla FC ni mabingwa mara nyingi wa michuano ya Europa na ujio wao utaongeza hamasa iliyoanzishwa na Everton hapa nchini, Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti wa SportPesa Tanzania,Tarimba Abbas kuona kila Mtanzania anapenda mchezo wa soka na kutokana na hilo wameweka viingilio vya Sh5,000 na Sh15,000 ili kuwavutia mashabiki na kuujaza uwanja huo. Tiketi hizo zinapatikana kwa mawakala wa Selcom na vituo vya mafuta vya Puma.
Mzee Muchacho na Fahad wambananisha Haji Manara avae jezi ya Yanga SC