Michezo

Shabiki kakasirishwa na Amunike kumuita Ajibu Taifa Stars “Anampeleka kwenye matatizo”

on

Kocha mkuu wa Taifa Stars Emmanuel Amunike ametaja kikosi hicho lakini ana mtihani wa kuhakikisha anafanya maamuzi sahihi kwa kuchuja majina 23 ya kikosi cha mwisho kitakachoshiriki fainali za AFCON 2019 nchini Misri, hivyo kati ya majina 39 atatakiwa kukata majina ya wachezaji 16 na kubakiza 23.
.
Sasa baada ya Ibrahim Ajibu kutajwa moja kati ya wadada wanaoishabikia Yanga amekasirishwa na kusema kwa nini wamemuita kwa sasa? kwa sababu wanampeleka kwenye matatizo yaani Misri akiamini Taifa Stars inaweza isifanye vizuri.
.
Hadi Amunike ameamua kumuita Ajibu ni kutokana na mchezaji huyo kuonesha uwezo mkubwa katika mechi za Ligi Kuu huku akiwa anaongoza kwa kutoa assist yaani pasi za usaidizi wa goli 11 TPL, Tanzania itashiriki fainali za AFCON mwezi June nchini Misri wakiwa wamepata nafasi hiyo kwa mara ya kwanza baada ya miaka 39.

Amunike kaita 39 Taifa Stars, kataja kigezo kitakachotumika kupata 23 AFCON 2019

Soma na hizi

Tupia Comments