Mshambuliaji wa club ya LA Galaxy ya Marekani ambaye amewahi kucheza vilabu mbalimbali barani Ulaya kwa mafanikio Zlatan Ibrahimovic, amepinga kauli ya nahodha wa timu ya taifa ya Ureno na staa wa club ya Juventus ya Italia Cristiano Ronaldo kuhusiana na kauli aliyoitoa alipokuwa anahamia Juventus.
Ronaldo wakati anahama Real Madrid na kujiunga na Juventus alitaja sababu inayomfanya ahame ni kutokana na kuamua kwenda Italia kutafuta maisha na changamoto mpya katika club nyingine, kauli hiyo Zlatan hajakubaliana nayo na kusema kuwa kama Ronaldo alikuwa anataka chalenji angejiunga na timu ya daraja la pili na kuipandisha Ligi Kuu na kuipa taji na sio kwenda katika timu iliyoshinda mataji tayari.
“Cristiano Ronaldo anaita ni changamoto mpya kwake kwenda kwenye timu ambayo tayari ilishajipambania na kushinda mataji ya Serie A miaka kadhaa nyuma, kama anataka changamoto kwa nini asingeenda katika timu ya daraja la pili na kuisaidia kupanda Ligi Kuu na kuipa Ubingwa? kwenda Juventus sio changamoto”>>> Zlatan Ibrahimovic
Kauli ya Zlatan imekuja kama kumtetea Lionel Messi ambaye Cristiano Ronaldo mwezi December alimtaka mchezaji huyo kuhama Ligi na kwenda kucheza sehemu nyingine kupata changamoto mpya, Zlatan anasema ni bora Messi aendelee na maisha yake ndani ya FC Barcelona kama atapenda kufanya hivyo na hana cha kufanya ili athibitishe ubora wake yeye tayari ni bora.
Mpenja katangaza goli kabla ya kona kupigwa, ataomba kutotangaza game za timu yake