Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars anayecheza soka la kulipwa katika club ya KRC Genk ya Ubelgiji Mbwana Samatta, nyota yake inazidi kung’aa baada ya kuwa na kiwango cha juu zaidi msimu huu akiichezea KRC Genk na kuwa kinara wa ufungaji magoli katika Ligi Kuu ya Ubelgiji ‘Jupiter Pro League’
Samatta leo kupitia mtandao wa hitc.com umetaja jina lake kuwa katika rada za club ya Cardiff City ya England kutaka kumsajili kutoka club ya KRC Genk ya Ubelgiji, Cardiff waliyopo katika nafasi za hatari katika Ligi Kuu England, wanamuhitaji Samatta aongeze nguvu katika timu yao ili kuinusuru na janga la kushuka daraja.
Cardiff wameripotiwa kutuma ofa ya pound milioni 11.6 ambazo ni zaidi ya Tsh Bilioni 34.3 kwa club ya KRC Genk ili kumpata Samatta lakini limekataliwa dau hilo, hivyo labda warudi na ofa ya pili kuishawishi Genk kumuachia Samatta, Samatta ambaye ameisaidi Genk kuongoza Ligi kwa tofauti ya point 7 akiwa anaongoza kwa ufungaji Jupiter Pro League, msimu huu amefunga jumla ya magoli 24 katika mashindano yote akicheza michezo 31.
Mpenja katangaza goli kabla ya kona kupigwa, ataomba kutotangaza game za timu yake