Premier Bet
TMDA Ad

Michezo

DoneDEAL: Abdallah Shaibu ‘Ninja’ uso kwa uso na Zlatan Ibrahimovic

on

Beki wa kati wa club ya Dar es Salaam Young Africans Abdallah Shaibu maarufu kama ‘Ninja’ pamoja na kutopewa kipaumbele katika timu aliyokuwa anaitumikia ya Yanga na kutojua hatma yake, mambo yameendelea kunyookea na kupata dili ambao halikutarajiwa na kila mmoja.

Yanga SC ilimuachia Ninja hadi mkataba wake unamalizika June 2019 bila kumpa ofa, ila baadae Ninja akapata timu Jamhuri ya Czech ya Ligi daraja la tatu inayojulikana kwa jina la MFK Karvina, timu hiyo imempa Ninja mkataba wa miaka minne na kumtoa kwa mkopo wa mwaka mmoja katika club ya LA Galaxy ya Ligi Kuu ya Marekani.

Kwa taarifa hiyo ni wazi sasa Ninja anayedaiwa kuwa atakuwa akilipwa msahara wa euro 18000 kwa wiki (zaidi ya Tsh milioni 45), anaungana kikosi kimoja na staa wa zamani wa Man United na Sweden Zlatan Ibrahimovic anayeitumikia club hiyo, Ninja na Zlatan sasa watakuwa wanashea chumba kimoja cha kubadilishia nguo (dressing room) na staa kama Zlatan.

Zlatan Ibrahimovic

KOCHA ZAHERA KIKOSI KAMILI KAWEKA NJE KINAISUBIRI TOWNSHIP ROLLERS

Soma na hizi

Tupia Comments