AyoTV

Sauti Sol hawatomuimba Rais Magufuli sema kuna kitu wamemkubali

on

Sauti Sol ni kundi la waimbaji wakali wa muziki wa kizazi kipya kutokea Kenya, ngoma zao zilianza kuwashika Watanzania toka kitambo mpaka sasa na moja ya ngoma zao zilizolia sana Tanzania ni ‘sura yako’

Pamoja na kwamba wanadili sana na muziki haimaanishi kwamba hawafatilii siasa, wameanza kuzifatilia siasa za Tanzania kwa ukaribu zaidi baada ya kusikia kuhusu Rais Magufuli.

Kwenye Exclusive Interview na millardayo.com & AyoTV wamesema…Tunapenda utendaji wake, Tanzania mkiendelea hivyo mtafika mbali sana, mimi aliniacha hoi pale alipofika Airport kukagua tu mara hii mashine imekuaje yaani huyu mzee yuko serious kuhakikisha rushwa haipo’

Kwa Afrika kupambana na vitu kama rushwa lazima tuwe na kiongozi kama huyu, na hata kabla ya Magufuli hajawa Rais alikua waziri wa ujenzi na tulikua tunamuheshimu sana na tulikua tunasikia kwamba Tanzania kuna Waziri flani, yani sifa zake zimeenea‘ – Sauti Sol

Unaweza kuwatazama Sauti Sol kwenye hii video hapa chini….

ULIIKOSA HII YA RAIS MAGUFULI JUZI SHINYANGA VS JAMES LEMBELI? ITAZAME KWENYE HII VIDEO HAPA CHINI

Soma na hizi

Tupia Comments