Premier Bet
TMDA Ad

Michezo

Asamoah Gyan katii ombi la Rais na kufuta uamuzi wake

on

Baada ya kuenea kwa habari katika mitandao ya kijamii kuwa mshambuliaji wa kimataifa wa Ghana Asamoah Gyan ametangaza kustaafu kuichezea timu ya taifa ya Ghana kuelekea michuano ya mataifa ya Afrika AFCON 2019 itakayofanyika Misri kutokana na kuvuliwa unahodha hatimae amebadili mawazo hayo.

Asamoah amebadili mawazo hayo baada ya Rais wa Ghana, Nana Akufo-Addo kumuomba afute uamuzi huo na kuamua kurejea timu ya taifa kama ilivyokuwa awali, Asamoah kwa heshima ya taifa lake na Rais wa nchi yake ameamua kubadili maamuzi hayo na kuamua kurudi.

Kwasi Appiah

Awali iliripotiwa kuwa Asamoah Gyan hataki kuwa chini ya kocha Kwasi Appiah ambaye amemvua unahodha kwa madai kuwa alifuatwa na mchungaji aliyedai kaoteshwa kuwa akimvua Gyan kitambaa cha unahodha ndio timu ya taifa ya Ghana itatwaa AFCON hivyo Asamoah alikerwa na taarifa hizo.

Mapokezi ya Sevilla Tanzania waliokuja kukipiga na Simba SC

Soma na hizi

Tupia Comments