Habari za Mastaa

Mahakama yaamuru Neyo kulipwa Tsh Bil.13 na meneja wake wa zamani

on

Kwa mujibu wa mtandao wa ‘The Blast’ umeripoti kuwa meneja wa zamani wa mwimbaji Neyo amepewa amri na Mahakama nchini Marekani ya kumlipa mwimbaji huyo kiasi cha dola za Kimarekani Mil.6 sawa na zaidi ya shilingi Bilioni 13 za Kitanzania.

Kevin Foster ambaye alikuwa meneja wa biashara za Neyo pamoja na Brian McKnight ameamuriwa kulipa kiasi hicho, pia atamlipa Brian kiasi cha dola za Kimarekani $151,675 sawa na zaidi ya shilingi Milioni 300 za Kitanzania, hiyo ni adhabu ambayo amepewa Kevin baada ya kudaiwa kuwa aliiba baadhi ya pesa wakati akiwafanyia kazi wawili hao.

Inaelezwa mwanzoni wa mwezi huu Kevin Foster amehukumiwa kufungwa miezi 89 jela baada ya kugundulika kuwa alimshauri Neyo kuanzisha biashara ya mgahawa ambapo alisema utagharimu mamilioni ya pesa na mkataba ulionekana kuwa feki na kukimbia na pesa hizo.

VIDEO: MOSE IYOBO HAJATOKEA KWENYE BIRTHDAY YA MWANAE, AUNT EZEKIEL KAZUNGUMZA

Soma na hizi

Tupia Comments