Wekundu wa Msimbazi Simba leo Alhamisi ya September 21 2017 walikuwa Mwanza katika uwanja wa CCM Kirumba kucheza mchezo wao wa nne wa Ligi Kuu Tanzania bara msimu wa 2017/2018 dhidi ya Mbao FC.
Simba ambao waliingia katika uwanja huo kwa tahadhari kubwa kutokana na Mbao FC kuwa na historia ya kuwasumbua, wamejikuta wakiambulia sare ya kufungana magoli 2-2 licha ya kuongoza kwa 2-1 hadi dakika ya 80.
Magoli ya Simba yalifungwa na Shiza Kichuya dakika ya 16 na James Kotei dakika ya 48 wakati magoli ya Mbao FC yalifungwa na Habib Kiyombo 45 na Boniface Maganga dakika ya 81, Simba ndio mara ya kwanza inashindwa kutoka na ushindi dhidi ya Mbao FC wakiwa wamewahi kucheza michezo mitatu.
Katika michezo hiyo mitatu ya mashindano yote Simba aliyocheza dhidi ya Mbao FC alifanikiwa kushinda yote ya Ligi Kuu alishinda 1-0 mchezo wa kwanza na CCM Kirumba akashinda kwa 3-2 na mchezo wao wa mwisho wa fainali ya FA katika uwanja wa Jamhuri Dodoma na Simba kupata ushindi wa 2-1.
ALL GOALS: Simba vs Mwadui FC September 17 2017, Full Time 3-0