AyoTV

CHADEMA imethibitisha Ester Bulaya kukamatwa na Polisi leo

on

Moja ya taarifa zinazomake headlines ni pamoja na hii ambayo kuhusu Mbunge wa Bunda Mjini na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Ester Bulaya kukamatwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Rorya katika Mkoa wa Mara akiwa katika majukumu ya kichama.

Bulaya imethibitishwa na Msemaji wa CHADEMA Tumaini Makene kuwa amekamatwa akiwa akiwa katika Hoteli aliyofikia Tarime ambako alikwenda kwa ajili ya shughuli za kichama.

Ayo TV na millardayo.com zimempata msemaji wa CHADEMA, Tumaini Makene:>>>”Ni kweli tumepata taarifa muda sio mrefu kwamba Mbunge wetu Jimbo la Bunda Mjini ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu Ester Bulaya amekamatwa na Jeshi la Polisi akiwa Hotelini kwake, Tarime. Alikuwa katika shughuli za kichama akiwa kama Mbunge na Mjumbe wa Kamati Kuu.”

ULIPITWA? Ester Bulaya kufungua kesi dhidi ya Wasira? Aomba ushauri Jimboni…tazama hapa chini!!!

Play kwenye video hii hapa chini kumtazama Mbunge Ester Bulaya akifunguka kuhusu gharama alizotumia kesi yake na Wasira…

Soma na hizi

Tupia Comments