Premier Bet
TMDA Ad

Habari za Mastaa

Kodak Black afunguliwa shtaka lingine akiwa gerezani

on

Kwa mujibu wa mtandao wa ‘The Blast’ umeripoti kuwa Rapper Kodak Black amefunguliwa mashtaka na promota baada ya kushindwa kutumbuiza kwenye tamasha alizopangiwa kwa mara kadhaa na kuvunja makubaliano aliyokuwa ameyaweka ndani ya mkataba. 

Promota huyo aliyetambulika kwa jina la Nicholas Fitts amedai kuwa rapper huyo amekuwa akitoa ahadi na kushindwa kuzitekeleza na kusema kuwa Kodak Black alishindwa kutumbuiza kwenye tamasha lililopangwa kufanyika March 3,2017 mjini New York lakini hakuonekana na baadae aliomba kupewa tarehe nyingine kulifanya tamasha hilo akapewa mwezi April,2017.

Nicholas Fitts aliamua kumpa nafasi ya tatu baada ya  kutoonekana kwenye matamasha hayo mawili na hakutokea hivyo amesema kuwa Kodak alivunja makubaliano hayo na anadai fidia ya shilingi Bilioni 1 za Kitanzania.

Inaelezwa pia kwa sasa rapper huyo yupo gereza la FDC Miami akitumikia kifungo cha miaka kumi akiwa na kesi ya kumiliki silaha kinyume na sheria pamoja na kudaiwa kusababisha maafa U.S. Marshals na silaha hizo.

VIDEO: MALKIA KAREEN AZUNGUMZA VILIO VYA MATUSI INSTA, SAFARI YAKE NJE, BONYEZA PLAY HAPA CHINI

Soma na hizi

Tupia Comments