Takriban Watu 21 wamefariki Dunia kufuatia mvua yenye baridi na upepo mkali wakati wanakimbia Ultra Marathon katika Jimbo la Gansu, Kaskazini Magharibi mwa China.
Maafisa wa eneo wanasema mbio hizo zilizojumuisha Watu 172 ziliathiriwa ghafla na hali mbaya ya Hewa ambapo ndani ya kipindi kifupi joto lilipungua na kutokea mvua yenye barafu.
Washiriki kadhaa walituma ujumbe wakiomba msaada na kufuatia hali kuendelea kuwa mbaya waandaaji waliahirisha mbio hizo na kutuma timu za waokoaji.