Halmashauri kuu ya CCM Taifa imempitisha Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa mgombea pekee wa nafasi ya mwenyekiti wa CCM Taifa kwa mwaka 2022 hadi 2027 na jina lake litapelekwa kwenye mkutano mkuu siku ya kesho Desemba 07 kwaajili ya kupigiwa kura
Na kwa nafasi ya makamu mwenyekiti halmashauri kuu imempitisha Abdullahman Kinana kuwa mgombea kwa kiti cha makamu mwenyekiti bara na Dkt. Hussein Mwinyi kwa upande wa visiwani Zanzibar
Taarifa hiyo ya chama imetolewa na katibu wa siasa itikadi na uenezi wa Chama hicho Shaka Hamdu Shaka akizungumza na vyombo vya habari leo Desemba 06,2022 wakati akitoa taarifa ya kuelekea mkutano wa 10 wa chama hicho Desemba 07 na 08 jijini Dodoma.