Premier Bet
TMDA Ad

Habari za Mastaa

Amber Rose mbioni kupata mtoto mwingine na Alexander Edwards

on

Mwanadada Amber Rose anatarajia kupata mtoto wake wa pili ambaye atakuwa wa kwanza pamoja na mpenzi wake mpya Alexander Edwards. Amber Rose ametangaza hilo kupitia ukurasa wake wa instagram saa kadhaa zilizopita akiwa hospitali.

Amber ameitaja jinsia ya mtoto huyo kuwa ni wa kiume, huyu anakuwa mtoto wake wa pili wa kiume, wa kwanza ni Sebastian aliyezaa na Rapper Wiz Khalifa.

Inaelezwa Amber Rose pamoja na Alexander walianza mahusiano yao ya kimapenzi miezi kadhaa iliyopita.

“Alexandra pamoja na mimi tunayo furaha kubwa kuwatangazia kuwa mtoto wetu wa kiume yupo njiani, sebastian ana furaha sana kuwa kaka mkubwa” >>>Amber Rose

AUDIO: ULIPITWA NA HII YA MUIGIZAJI WEMA SEPETU KUHUSU MAMA YAKE MZAZI? BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUSIKILIZA MWANZO MWISHO

Soma na hizi

Tupia Comments