Habari za Mastaa

PICHA 14: Patoranking alivyosherekea uzinduzi wa Album yake ‘Wilmer’

on

Fahamu kuwa usiku wa kuamkia leo May 21,2019 ilifanyika sherehe ya kusikiliza ngoma ambazo zinapatikana ndani ya album mpya ya mwimbaji Patoranking kutokea Nigeria ikiwa jina la album hiyo ni Wilmer , mastaa mbalimbali walihudhuria akiwemo Phyno, Wizkid, Tiwa Savage, Deejay Neptune, D’Banj

Inaelezwa kuwa album hiyo ya Wilmer imepangwa kuachiwa rasmi May 24,2019 na ndani yake mastaa kibao wameshirikishwa kwenye ukamilishaji wa ngoma tofauti tofauti akiwemo Davido, Nyashinski(Kenya) , Bera (Ufaransa), Dadju (Congo), Busiswa (Afrika Kusini) na Donae’o (Uingereza).

“Nimeweka moyo na nafsi yangu kwenye hii Album, Wilmer amekua ni baraka na ninatumaini huu mradi  utawahimiza , kuwahamasisha na kuwabariki. Safari haikuwa rahisi lakini tunashukuru kwa tunapoelekea, Mungu ambariki kila mmoja ambaye amekuwa msaada kwenye hili” aliandika Patoranking kupitia ukurasa wake wa instagram.

 

AUDIO: PIERRE LIQUID NDANI YA KISARAWE AKABIDHI MADAWATI, BONYEZA PLAY HAPA CHINI 

Soma na hizi

Tupia Comments