Habari za Mastaa

Vanessa Mdee kuileta Album yake ya pili, Producer wa Beyonce na Nicki Minaj kahusika

on

Mwimbaji Vanessa Mdee ametudokeza ujio wa album yake ya pili baada ya Album ya ‘Money Mondays’ kufanya vizuri ndani na nje ya Tanzania tokea iachiwe January 15, 2018, kupitia insta story ya Vanessa ameziweka good news hizo akiwa bado yupo nchini Marekani.

Vanessa Mdee ameweka wazi na kuandika kuwa mpaka sasa album hiyo imekamilika kwa asilimia 70 na amefanikiwa kuingia studio na vocal producer maarufu duniani Nick Cooper ambaye anafanya vocals za mastaa wakubwa nchini Marekani  kama Beyonce, Nicki Minaj na JLo

“Leo nimebahatika kuingia studio na vocal producer maarufu duniani Nick Cooper @vcs_laambaye anafanya vocals za kina Beyonce, Nicki Minaj, JLO … lets just say ALBUM NUMBER 2 is going to be LIT 🔥” >>>Vanessa Mdee

 

UMEPITWA NA HII YA PIERRE LIQUID ALIVYOTUA BUNGENI DODOMA? BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA MWANZO MWISHO

Soma na hizi

Tupia Comments