Mchekeshaji Eric Omondi kutokea nchini Kenya amefunguka mengi kuhusiana na tasnia ya uchekeshaji hasahasa watu wanapotambua kuwa mtu ni mchekeshaji na kusema kuwa endapo mtu akifahamu hivyo anategemea kupata vitu vya kuchekesha kutoka kwako.
Eric Omondi ambaye ni mshindi wa tuzo ya mchekeshaji bora Afrika 2018 ameyaongea hayo katika radio ya Virgin Dubai kwenye kipindi cha ‘This is the Kris Fade Show’ alipokuwa Dubai kwenye sherehe za Global Comedy Festival zilizofanyika usiku wa November 15,2018 na kusema kuwa alianza uchekeshaji akiwa na umri wa miaka mitano.
“Nilienda Marekani pale Times Square na nikavaa kama mganga wa kienyeji huku nikiwa nimebeba mboga mboga tu kama kabichi wazungu walikuwa wakinishangaa na nilikuwa nikizungumza kiswahili na nikawaambia hii ni dawa ya asili na inatibu magonjwa yote na ina gharimu elfu 40 na biashara hapohapo ikakua”
“Show kubwa ambayo niliwahi kufanya ni pale Kitale Kenya na kujaza watu elfu 44, nilianza kazi hii ya uchekeshaji nikiwa na miaka mitano nilikuwa mtundu sana sikutaka kuona mtu hana furaha nilijaribu kila njia kuona mtu ana furaha” >>>Eric Omondi
DC Jokate alivyotaja sifa tatu kuhusu Waziri Mhagama ‘Wewe ni mrembo sana’