HekaHeka

Umeisikia hii ya mwanamke kuolewa mara mbili? Mume wa pili hata hakujua.. #HEKAHEKA

on

Rings-on-FingersIshu ni kwamba kuna mwanaume alikutana na msichana wakapeana namba za simu wakawa wanawasiliana, wakaanzisha uhusiano, baadae wakafunga ndoa.. kilichoibuka baadae kumbe yule mwanamke ni mke wa mtu !!

Mwanaume huyo amesema alipokutana na mwanamke huyo alimwambia kuwa ni mwanafunzi  wa kidato cha tatu, wakaendelea na uhusiano hadi binti alipomueleza kuwa amemaliza shule na kujiunga VETA, akasoma mpaka akamaliza. uhusiano wao ulidumu kwa miaka miwili, hakuna tatizo lolote lilitokea hapo katikati.

Wakakubaliana waoane.. Mwanaume akapeleka barua ya posa kwa wazazi wake na harusi ikafungwa nyumbani kwao Zanzibar.

Wakiwa ukumbini wazazi wa mwanaume wakasikia tetesi kuwa mwanamke huyo ameolewa na ana familia yake.. wakaanza kufuatilia na kugundua kuwa mwanamke huyo ameolewa na ana watoto wanne, yuko kwenye ndoa kwa miaka 16.. ndoa hii mpya haikwenda mbali, ilivunjika ndani ya wiki moja.

Hekaheka imeishia hapo leo, lakini Geah Habib ameahidi muendelezo wake utakkuwa kesho mtu wangu.. Hii unaweza kuisikiliza hapa.


Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>>  Twitter Insta FB  na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>> Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

Soma na hizi

Tupia Comments