Kwenye kipindi cha Leo Tena walikuwa wanapiga story na viongozi wa bendi za FM Academia na Twanga Pepeta ambapo kiongozi wa FM Academia, Nyoshi El Sadat amesema kilichomfanya apendelee kuvaa wigi ni kutaka kuwa na muonekano wa tofauti.
Nyoshi amesema kuvaa wigi iliwahi kumletea Hekaheka kutokana na watu wengi kufikiria tofauti huku wengine wakimwambia wigi analovaa lina uhusiano na masuala ya imani za kishirikina ili bendi yake ifanye vizuri.
Sikuwahi kujua kwamba kumbe Nyoshi amekuwa akivaa mawigi kwa muda wa miaka 15, lakini ameacha miezi miwili iliyopita kwa sababu anataka awe na muonekano tofauti na mashabiki zake wamefurahia muonekano wake mpya.
Nyoshi ana story nyiiingi mtu wangu, play hapa umsikie yani…
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia Twitter, Instagram na Facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza>>>twitter Insta Facebook