Hekaheka leo inazungumzia ndoa ya mwanamuziki wa Mashauzi Classic Hashim Said ambaye alitengana na mke wake Zai mara mbili lakini sasa wanaishi pamoja.
Mke wake amesimulia kwenye hekaheka ya leo na kusema kabla ya kutengana na mume wake..kitu ambacho hatakisahau kuna siku mume wake alimuaga anakwenda mazoezini lakini hakurudi hadi majira ya sana nane usiku..anasema alimtafuta sana kwenye simu lakini hakumpata..lakini akaja kujua alikuwa na uhusiano na mwanamke mwingine.
Anasema baada ya kurudi nyumbani usiku sana, kesho yake asubuhi mume wake akampa talaka..baada ya siku tatu akasikia anaoa..hakuamini kilichotokea na siku ya harusi ya mume wake aliamua kwenda kama mgeni mwalika baada ya sherehe kwisha akarudi nyumbani.
Baada ya misikusuko mingi walikuja kurudiana na sasa wanaishi maisha ya uaminifu katika ndoa yao..
Wasikilize hapa Hashim na mke wake wakisimulia changamoto zao kwenye Hekaheka…
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenyeTwitter,FB,Instagram na YouTUBE kwa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAM, TWITTER,FB, YOUTUBE