Premier Bet
TMDA Ad

HekaHeka

Leo mwanaume kasimulia alivyoachwa na mke wake alafu akaenda kuolewa mara ya pili..

on

Isolated-man-looking-out-at-pier

Kwenye show ya LEO TENA ambayo huwa inasikika #OnAiR kila siku on @CloudsFM huwa kunakua na Hekaheka pia.. zinatoka mtaani kwenye maisha ya kawaida ya kila siku yani, iliyosikika leo ni mwendelezo wa kilichosikika jana, mwanamke mmoja kaolewa mara mbili, yani katoka kwenye ndoa ya kwanza kwenda kwa mwanaume mwingine.

Kilichosikika jana ni kwamba mvulana ambaye alimuoa mara ya pili alisema kwamba mwanamke huyo alimdanganya kwamba anasoma kidato cha tatu, wakaendelea na uhusiano mpaka wakafikia hatua ya kuoana, masheikh walishtukia katikati ya shughuli kwamba mwanamke huyo ameolewa na ana watoto wanne, leo aliyesikika kwenye Hekaheka ni mume wake wa kwanzaanasimulia jinsi ambavyo mke wake aliondoka.

Mwanaume huyo amesema hawakuwahi kuwa na ugomvi siku za nyuma, alishangaa kuona mke wake anadai talaka ghafla bila sababu, baadae akasikia kwamba ameolewa na mwanaume mwingine.

Mume huyo amesema kamsamehe lakini hayuko tayari kurudiana nae.. Mwanamke huyo alikoolewa ndoa haikukamilika, masheikh waliizuia kutokana na mwanamke huyo kushtukiwa kwamba hakufuata taratibu ili aolewe ndoa ya pili.

Najua utakua na hamu kumsikia mwanaume huyo akiongelea ishu ya kuachana kwao, bonyeza play hapa uisikie Hekaheka yote..

Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>>  Twitter Insta FB  na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa>>>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

 

Soma na hizi

Tupia Comments