Hekaheka ya leo itakua tofauti kidogo na ambazo tumekuwa tukiwaletea kila siku.
Leo Musa Hussein kapiga stori na Mtayarishaji wa leo Tena Michael Lukindo pamoja na Jose Mara ambaye amezungumzia maisha yake kabla ya kujiunga na bendi ya Mapacha watatu.
Lukindo amezungumza na kusema zamani akiwa Arusha wakati wanaanza kazi ya uandishi wa habari, walianzia kazi kwenye gazeti moja ambalo kwa sasa limefungwa, wakati wanatafuta stori wakakutana na rafiki wa bosi wao, akasema walitengenezewa mtego na bosi wao wakidaiwa kupokea pesa za matangazo kwenye gazeti kinyume na utaratibu na kujikuta wakiishia mikononi mwa Polisi.
Kingine Jose Mara amesema kabla ya kujiunga Mapacha watatu wakati akiwa na bendi ya FM Academia …muhasibu wao alipewa kazi ya kwenda kuwatafutia nyumba za kuishi na kupata maeneo ya Msisiri…amesema eneo hilo lilikuwa ni uswahilini sana na kukuta mambo ya kiswahili ikiwemo kila mwaka wapangaji kutakiwa kucheza ngoma za kupandisha mashetani.
Anasema siku moja wakati anatoka kwenye show zao akiwa anarudishwa nyumbani na gari la ofisi alikuta majirani zake wakicheza ngoma na walipomuona wakapandisha mashetani na kuanza kumfukuza.
Msikilize hapa Lukindo na Jose Mara wakizungumza na Musa Hussein…
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenyeTwitter,FB,Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAMTWITTERFBYOUTUBE.