Kwenye yale matukio ya hekaheka leo inawahusu vijana wawili raia wa Yemen ambao walikuja Tanzania baada ya kukimbia machafuko nchini kwao huku mmoja akiwa na jeraha kubwa baada ya kupigwa na bomu.
Vijana hao walifikia kwa ndugu yao aliyekuwa akiishi Magomeni ambaye aliahidi kukaa nao na kumtibu mmoja wao mpaka atakapopona na jana ndio ilikua siku yao ya kurudi kwao.
Hekaheka ilianzia pale vijana wale walipotakiwa kuondoka ghafla huku wakiwa hawajapewa taarifa na kuanza kuangua vilio wakigoma kurudi kwao huku baadhi ya majirani wakiwatetea na kuahudi kuwasaidia lakini ndugu yao alikataa wabaki na kusababisha watu kujazana
Mmoja wa majirani amesimulia na kusema mmoja wao alipigwa bomu akiwa Yemen wakati wa vita na hawakuwa tayari kurudi baada ya kutakiwa kufanya hivyo na kaka yao aliyekuwa amewahifadhi…waliishi vizuri ingawa hawakua wakijua kiswahili.
Wasikilize hapa…
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia kuanzia kwenye siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos