Idara ya Hekaheka leo imepiga Stori na msanii Barnaba, unajua mastaa wanakutana na visa vingi sana kwenye maisha ya kila siku wanayoishi, Barnaba kaamua kushea hiki kimoja kilichomkuta akiwa na Alawi Junior.
Barnaba anasema kuna siku moja alikua na Alawi Junior wakiwa katika mishemishe za kuachia wimbo wao, wakiaenda kwa mshkaji mmoja ili wapige picha kwa ajili ya kutengenezea cover ya wimbo.
Ishu ikawa pale ambapo mpiga picha alidai awapime vipimo wakiwa wamefumba macho kabla ya kupigwa picha.. Barnaba akaona hapa hakuna biashara tena, akagoma kabisa kwa sababu hakuona sababu ya kufanyiwa vipimo vyovyote kabla ya kupiga picha.
Msikilize hapa mtu wangu…
Unahitaji chochote nachokipata kikufikie? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.