Club ya AS Monaco ya Ufaransa leo usiku wa January 24 2019 imetangaza rasmi kumsimamisha kazi kocha wake mkuu wa timu hiyo raia wa Ufaransa Thierry Henry, Henry amesimamishwa kazi baada ya jahazi la timu hiyo kuzidi kudorora hivyo mabosi wanahofiwa timu kushuka daraja.
Thierry ambaye amekuwa kocha wa AS Monaco kwa muda sasa amekuwa na wakati mgumu kupata matokeo akiwa na timu hiyo, zaidi imekuwa ikipoteza zaidi, uongozi umeamua kumsimamisha ili wajadili hatma ya kocha huyo katika kikosi chao.
Toka awasili Thierry mwaka 2018 mwisho katika timu ya AS Monaco ameiongoza katika game 2o na kufanikiwa kushinda game 4, sare game 5, wamepoteza game 11, timu imefunga magoli 15 katika michezo 20 na kufungwa magoli 36 na kwa sasa ipo nafasi za hatari kushuka daraja nafasi ya 19 wakiwa na point 15 tofauti ya point tatu aliyekuwepo na nafasi ya 17 ya kutoshuka daraja.
VIDEO: Mwalimu Kashasha kuhusu pasi ya Ajibu kwa Fei Toto “Locomotive faint”