Leo February 6, 2018 katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania suala la mgongano wa kikatiba na kimamlaka kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar limejitokeza bungeni baada ya kuibuliwa na Mbunge wa Wangwi, Juma Kombo Hamad.
Hali hiyo ilijitokeza katika kipindi cha maswali na majibu bungeni Dodoma baada ya Mbunge huyo kutaka kufahamu ni lini Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itapeleka mapendekezo ya mabadiliko ya katiba bungeni ili kuondoa changamoto zinazotajwa kuwemo katika katiba hizo.
Kufuatia swali la Mbunge Juma Kombo Hamad, Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi amesema Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ile ya Serikali ya Zanzibar hazina mgongano na hivyo kutoona haja ya kupeleka mapendekezo ya kubadili katiba hizo kama mbunge huyo alivyoomba.
Profesa Kabudi amesema, Muungano wa Tanzania ni miongoni mwa Muungano wa kipekee Duniani kutokana na Katiba zake kuwa wazi na kuwa na mashirikiano mengi katika masuala muhimu kwa mustakabali wa Taifa na nchi zote mbele bila kuleta mgongano wa kimamlaka wala kikatiba
Via Azam Tv
MBUNGE MALECELA KUHUSU WANAOSEMA SERIKALI YA MAGUFULI HAIJAFANYA LOLOTE, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA