Winga wa zamani wa club za Ajax, Arsenal na FC Barcelona Marc Overmars amenukuliwa na vyombo vya habari akitoa kauli kuwa staa wa Man United Alex Sanchez baada ya kuwa na wakati mgumu ndani ya club ya Man United ana mipango ya kurudi kuichezea Arsenal.
Marc Overmars anaamini kuwa Sanchez atarudi tena Arsenal alipokuwa akiichezea kwa kiwango cha juu kwa miaka minnne, baada ya kuondoka msimu uliopita na kujiunga na Man United ambayo ndani ya mwaka huo mmoja ameichezea jumla ya gema 37 na kufunga magoli matano pekee, Marc Overmars ambaye pia ni director wa michezo wa Ajax amehoji maamuzi ya Sanchez kujiunga na Man United.
Mkongwe Marc Overmars ambaye ameshinda mataji matatu ya Ligi Kuu England akiwa na Arsenal 1997-2000, anaamini kuwa Alex Sanchez atajutia uamuzi wake huo wa kuihama Arsenal na kujiunga na Man United, kwani anaamini hakufanya maamuzi sahihi.
Imeshinda Simba SC tabu kaipata JB wakati wa kutoka