Michezo

Tottenham Hotspurs washitua wengi, kung’olewa na under dog Carabao Cup

on

Club ya Tottenham Hotspurs imeshitua mashabiki wengi wa soka baada ya kuondolewa katika michuano ya Carabao Cup dhidi ya Colchester ya Ligi, mchezo huo ulimalizika kwa sare tasa ya 0-0 lakini baada ya kwenda katika hatua ya mikwaju ya penati Tottenham wakapoteza kwa penati 3-4.

Kinachowashitua wengi katika mchezo huo ni kushindwa kufunga goli dhidi ya timu inayoonekana kama under dog (Colchester) ukilinganisha na Tottenham Hotspurs ambaye ni makamu Bingwa wa michuano ya UEFA Champions League msimu uliopita kwa maana ya kumaliza akiwa nafasi ya pili.

Kwa hadhi na viwangi vya wachezaji wa Tottenham waliaminika kuwa hawezi kuruhusu kufika hatua ya hatari ya mikwaju ya penati, ambayo kwa kawaida inategemea bahati zaidi, baada ya kutolewa katika michuano hiyo ambayo walikuwa wakitarajiwa kuwatatoa hata moja msimu huu, Tottenham 2019 inaingia ikiwa ni mwaka wao wa 10 bila kuwa na taji lolote.

VIDEO: Moja kati ya magoli ya marehemu Jeba, hili liliwaumiza wana-Simba 2016

Soma na hizi

Tupia Comments