Watu wengi walitaka kusikia kauli ya kocha kuhusu wazchezaji sita wa simba SC walioachwa Taifa Stars kwa kuchelewa kufika kambini kwa wakati walioitwa, kocha mkuu wa Taifa Stars Mnigeria Emmanuel Amunike ameongea na waandishi wa habari na kueleza kuhusiana na hatma ya wachezaji hao.
“Najua mnataka kusikia mfumo mnataka kusikia nani atacheza mechi ya uganda lakini katika mpira kuna vitu ambavyo ni maalum kwa ajili ya timu na huwezi kuweka wazi kila kitu”
“Pia nataka kuweka wazi kuhusiana na suala lililokuwa limetokea wakati wa kuanza kwa kambi ya Taifa Stars kuwa kuna wachezaji walipata mualiko lakini hawakufika kwa wakati hivyo tukalazimika kufanya maamuzi magumu ya kuwaondoa lakini haina maana wao sio sehemu ya timu wao ni sehemu ya timu ila katika taasisi yoyote ni lazima kujenga nidhamu”
Huo ndio msimamo wa kocha Amunike kwa wale ambao walikuwa wanajua kuwa wale walioachwa hawatoitwa Taifa Stars tena nafasi wanayo wakionesha uwezo tena lakini hawatokuwa sehemu ya timu katika mchezo dhidi ya Uganda pekee nikukumbushe tu wachezaji sita wa Simba SC walioachwa ni Shomary Kapombe, Hassan Dilunga, Jonas Mkude, Shiza Kichuya, Erasto Nyoni na John Bocco.
Mtazamo wa Madee kwa nini Messi na Griezmann hawakustahili tuzo za FIFA