Premier Bet
TMDA Ad

Michezo

Hii ndio first eleven ya Brazil Kombe la Dunia 2018, Firmino na Silva Out !!!

on

Bado miezi kadhaa tuweze kushuhudia fainali za michuano ya Kombe la dunia itakayofanyika nchini Urusi kuanzia mwezi June 2018, kocha wa timu ya taifa ya Brazil Tite kuelekea fainali hizo ametangaza kikosi chake cha kwanza yaani first eleven.

Kocha Tite mwenye umri wa miaka 56 ameweka wazi kuwa staa wa Liverpool Roberto Firmino hana nafasi katika kikosi cha kwanza pamoja na mwenzake Thiago Silva wa Paris Saint Germain ya Ufaransa lakini amesema kuwa wapo katika list ya wachezaji 15 wa kikosi cha kwanza ila sio First eleven.

Kwa mujibu wa kocha Tite aliyenukuliwa na UOL Esportes first eleven yake ni Alisson, Marcelo, Miranda, Marquinhos, Daniel Alves, Paulinho, Renato Augusto na Casemiro, Neymar, Coutinho na Gabriel Jesus.

Hiki ndio kikosi cha kwanza cha Brazil katika World Cup 2018 na idadi ya mechi za kimataifa alizocheza kila mchezaji.

Haji Manara amewasikia wanaoibeza Simba kutoka sare ya 2-2 vs Mwadui FC

Soma na hizi

Tupia Comments