Timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars usiku wa jana March 22 ilicheza game ya kirafiki dhidi ya timu ya taifa ya Algeria mjini Algers nchini Algeria na kupoteza kwa magoli 4-1, baada ya kipigo stori zilianza kuenea katika mitaani kuwa kocha amekina kikosi.
Afisa habari wa Simba Haji Manara ni miongoni mwa watanzania ambao wameufutilia kwa karibu mjadala unaoendelea katika mitandao ya kijamii kuhusiana na Taifa Stars kufungwa magoli 4-1 na Algeria, Manara ameamua kuandika ujumbe huu kuhusiana na kinachoendelea.
“Kila mmoja anasema lake..wapo wanaomlaumu kocha,wapo wanaobeza uteuzi sijui kuna majeruhi ndani ya kikosi, mimi mtazamo wangu ni tofauti kidogo..tushaajiri makocha kila sampuli nchi hii toka mabara tofauti..bado hatujafanikiwa”
“Kama Taifa kuna mahali tunakosea kisha hatujui kosa lenyew..narudia kunahitajika national debate kujua kwanza kiini cha kufeli kwetu kisha ndio tuchukue hatua.. @tanfootball@harrisonmwakyembe”
Hivi ndio Simba walivyotoka sare ya 2-2 dhidi ya Al Masry