Moja kati ya majina makubwa katika soka la bongo ambayo yamewahi kuchukua headlines ni winga wa zamani wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars ambaye anaichezea Ndanda FC ya Mtwara kwa sasa Mrisho Khalfan Ngassa.
Ngassa amechukua headlines na umaarufu mkubwa katika soka la Tanzania akivichezea vilabu vya Yanga, Simba SC na Azam FC kutokana na kiwango chake kikubwa alichowahi kukionesha kwa sasa Ngassa amepoteza namba timu ya taifa, ila leo ameandika ujumbe huu kwenye ukurasa wake wa instagrama.
“#mwambawaziwavictoria kuna muda wakusifiwa kuna muda wa kuzomewa wanao kushangilia Leo kesho wakikuzomea usiwapige Bali jiulize ulicho wakosea mpaka kukuzomea kisha ukipata jibu utafanya wakushangilie tena ni mawazo yangu 2 mchana mwema Enjoy soccer”>>> Ngassa
UTANI MWINGINE HUU: Mkaliwenu baada ya sare ya 2-2 ya Simba SC vs Al Masry