Usiku wa Vikings uliofanyika King Solomon siku ya Jumamosi March 10,2018 mastaa mbalimbali walijitokeza kushuhudia kile ambacho Papii Kocha na baba yake Babu Seya waliandaa baada ya kutumikia miaka 13 jela.
Ukiongelea aina ya nguo”Fashion” ambazo mastaa walivaa usiku wa Vikings basi hauwezi kuacha kumtaja muigizaji Jacquline Wolper ambaye nguo yake ilizua maneno mengi katika mitandao ya kijamii ambapo wengi walisema kuwa amevaa parachuti.
Kupitia mtandao wa snapchat wa Jacquline Wolper alionekana kupata negative comments zilizokuwa zikitoka kwa mashabiki kutokana na wengi kusema amevaa parachute na amemuiga staa wa muziki nchini Marekani Cardi B baada ya kuonekana amevaa nguo iliyofanana na ya Jacquline Wolper.
“Nimevaa juzi Cardi B kavaa jana nimeambiwa nimeiga jamani wabongo pendeni vya kwenu, ninaweza sana mkubali mkatae hakuna designer asiyeiga lini maparachuti yangu sijawahi kuiga huwanapenda kupaa mwenyewe”
Ulipitwa na furaha ya Chege baada ya kupata mtoto?