Naibu waziri wa habari, utamaduni, sanaa na michezo Juliana Shonza leo amefanya mkutano na waandishi wa habari uwanja wa Taifa Dar es Salaam na kuzungumzia mambo mbalimbali kuhusu sanaa na kuzifungia nyimbo kadhaa za Bongofleva kwa madai ya kuharibu maadili.
Naibu waziri Shonza pia leo ametangaza kumfungia miezi sita kutojihusisha na muziki, wala kufanya show msanii Roma Mkatoliki kwa madai ya kukaidi wito wa BASATA, kutokana na kuimba wimbo wa Kibamia unaodaiwa kuwa hauna maadili.
Hata hivyo naibu waziri pia hakuishia kwa Roma pekee bali alisema kuwa wamempa onyo Nay wa Mitego kutokana na wimbo wake wa Makuzi na kuagiza pia aufanyie marekebisho wimbo wa Mikono Juu, kikubwa kilichomfanya Roma kupata adhabu hiyo ni kutoitikia wito.
Ni Ray vs JB ulingoni April 1 2018, JB ametangaza kulinda rekodi yake